Skip Global Navigation to Main Content
Skip Breadcrumb Navigation
Habari Kutoka Ubalozi

Balozi wa Marekani akabidhi ruzuku kwa vikundi vya kijamii

24, Agosti, 2015
Balozi wa Marekani akabidhi ruzuku kwa vikundi vya kijamii  (Picha kwa hisani ya Ubalozi wa Marekani)

Hapo tarehe 24 Agosti 2015, Balozi wa Marekani nchini Tanzania alikabidhi ruzuku kwa vikundi na mashirika ya kijamii 14 yanayofanya kazi ya kuboresha maisha ya Watanzania katika hafla iliyofanyika katika Ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam. Inatarajiwa kuwa ruzuku hiyo itawanufaisha moja kwa moja zaidi ya watu 5000 katika mikoa 12 humu nchini na itaboresha huduma na fursa katika sekta za maji na usafi wa mazingira, afya, elimu na maendeleo ya kiuchumi... (Habari Zaidi)

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari

  • Tamko kutoka Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania

    28 Oktoba, 2015

    Serikali ya Marekani imestushwa sana na tamko la hivi karibuni la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ambapo ametamka kusudio lake la kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais wa Zanzibar. Hatua hii inasitisha mchakato wa uchaguzi uliofanyika vizuri na kwa amani, kama ilivyo elezwa na waangalizi wa uchaguzi kutoka Ubalozi wa Marekani, Jumuiya ya Ulaya, Jumuiya ya Madola na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika pamoja na kusitisha zoezi la majumuisho ya kura lililokuwa linakaribia kukamilika. Tunatoa wito wa kuondolewa kwa tamko hilo  na kuzisihi pande zote kudhamira kwa dhati kuukamilisha mchakato huu wa kidemokrasia kwa uwazi na kwa Amani. Watu wa Zanzibar wanastahili jambo hilo.

Ripoti