Skip Navigation
Skip Left Section Navigation

Matukio Katika Picha

Balozi wa Marekani aungana na Wamarekani wengine kujitolea kujenga nyumba Korogwe

 

Siku ya Jumatano Januari 10 mwaka huu, Balozi wa Marekani nchini Michael
L. Retzer aliungana na Mbunge wa Marekani Steven Weickert kutoka Appleton,
Wisconsin, pamoja na Wamarekani wengine 14 wa kutoka jimbo la Wisconsin,
ambao hivi sasa wanatembelea Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga kusaidia
kujenga nyumba kwa watu wanaohitaji makazi. Mradi huu ni sehemu ya
mpango wa taasisi ya Habitat for Humanity Tanzania unaolenga kujenga
nyumba nzuri zenye gharama nafuu kwa wananchi wa Korogwe, ambao
hawana nafasi ya kupata makazi ya kuridhisha.

 Left: Ambassador Michael L. Retzer with a volunteer. (January 10, 2007)
Kushoto: Balozi Retzer na mmarekani wakujitolea. January 10, 2007.  
Wamarekani wakujitolea wakijenga pamoja na Mbunge wa Marekani Weickert.
(aliyewekea mgongo kamera) 
Wenye nyumba na wamarekani wakujitolea wakijenga pamoja.