Balozi wa Marekani hivi karibuni alizindua wilayani Longido mradi unaofadhiliwa na mfuko wa Balozi unaosaidia miradi midogo midogo, ambao uligharimu dola 5,383. Fedha hizo ziliwezesha shule tatu (Olkejuloongisho, Kiserian na Losirwa) kununua madawati 255. Madawati haya yanatumiwa na wanafunzi 510 kutoka familia za wafugaji wa Kimasai. Kwenye hafla hiyo, Balozi Retzer alikabidhi vitabu kwa watoto hao.
|
 |
Bi. Mollel, mwalimu wa shule ya Olkejuloongisho anaonekana akimvisha Balozi wa Marekani vazi la Kimasai. (Februari 19, 2007). |
Kutoka kushoto – Meneja wa Mradi Mike Ole Mokoro, Mkuu wa Wilaya ya Longido James Ole Milia na Balozi Retzer.
|