Matukio Katika Picha
Jenerali William E. “Kip” Ward, Kaimu Kamanda wa Kamandi ya Ulaya ya jeshi la Marekani atembelea Tanzania
| Jenerali William E. “Kip” Ward, Kaimu Kamanda wa Kamandi ya Ulaya ya jeshi la Marekani alikutana na Balozi wa Marekani nchini Michael Retzer; Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Prof. Juma Kapuya, Mkuu wa Majeshi Jenerali George Waitara; na viongozi wengine mjini Dar es salaam Machi 3, 2007. Mandumuni ya ugeni huo ni kujenga mahusiano na viongozi wa nchi na kupata mawazo yao kuhusu mambo ya sasa na ya baadaye ya ushirikiano kati ya Marekani na Tanzania. Ward na ujumbe wake unawatembelea viongozi wengine muhimu wa Burundi, Ethiopia, Rwanda, na Uganda. |
| |
| Wakiwa Ikulu ni (kutoka kushoto) Balozi Retzer, Jenerali Ward na Rais Kikwete. Machi 3, 2007. |
| Wakitoka Ikulu ni (kutoka kushoto) Balozi Retzer, Rais Kikwete na Jenerali Ward. |
| Waziri Kapuya akipokea zawadi kutoka kwa Jenerali Ward. More... |



