Skip Navigation
Skip Left Section Navigation

Kiswahili Editorial

Avian Flu in Egypt

January 17, 2007

Ndugu watatu wa familia moja wamefariki Misri baada ya kupata virusi vya H-5-N-1 vinavyoambukiza homa ya mafua ya ndege. Tangu mwezi Februari 2006 kumekuwa na ripoti ya kesi 18 na vifo kumi nchini Misri. Kote duniani, idadi ya kesi za ugonjwa huo tangu mwaka 2003 ni watu 261 ambapo watu 157 wamekufa.

John Rainford, msemaji wa Shirika la Afya Duniani - WHO - anasema vifo vya hivi karibuni Misri vilisababishwa na maambukizo kutoka kwa bata waliokuwa na ugonjwa huo. Lakini kama kirusi hicho kinaweza kugeuka katika hali inayoweza kuambukizwa kirahisi miongoni mwa binadamu mlipuko unaweza kuzuka dunia nzima na kuhatarisha mamillioni ya watu.

Homa ya mafua ya ndege imeingia katika nchi zaidi ya 50, na mamillioni ya kuku wamekufa au kuteketezwa katika hatua ya kuepusha kuenea kwa ugonjwa huo kwa ndege wengine.

Marekani imeahidi zaidi ya dolla millioni 434 katika juhudi za kimataifa kudhibiti ueneaji wa ugonjwa huo na kujitayarisha kwa uwezekano wa mlipuko miongoni mwa binadamu. Marekani inafanya utafiti na kuanda chanjo na madawa mengine. Marekani pia inashirikiana na Umoja wa Mataifa na mashirika mengine kuboresha ufuatiliaji wa ugonjwa huo.

Mwaka 2005, Rais George W. Bush alitangaza kuunda kwa ushirikiano wa kimataifa “kugundua na kuchukua hatua za haraka endapo mlipuko utatokea.”

”Mlipuko wa homa ya mafua utakuwa na matokeo mabaya kwa dunia. Hakuna taifa linaloweza kupuuzia tishio hili, na kila taifa lina wajibu wa kufuatilia na kuzuia ueneaji wake.”

Balozi John Lange, mwakilishi maalum wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani katika maswala ya milipuko ya magonjwa anasema, “kujitayarisha na kuongeza uwezo wa muda mrefu kunahitaji ushirikiano katika ngazi za kimataifa, kieneo, kitaifa na ngazi za kijamii.”