Skip Navigation
Skip Left Section Navigation

Kiswahili Editorial

Remembering Martin Luther King

January 17, 2007

Kiongozi wa harakati za haki za kiraia na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobeli, Martin Luther King Jr., aliwahi kusema, “ Ukosefu wa haki popote ni tishio kwa haki kila mahali”. Leo tarehe January 15, marekani inasherehekea sikukuu kwa heshima ya Dr King.

Wamarekani wanamuonyesha heshima mtu ambaye aligusa dhamiri ya taifa, alisema rais George W.Bush. Tunaikumbatia tena ndoto ambayo Dr King aliitolea maisha yake, Marekani ambako hadhi ya kila mtu inaheshimiwa; ambako watu wanapimwa siyo kwa msingi wa rangi yao bali tabia zao, na ambako tumaini la usoni bora lipo katika kila mtaa.

Dr King, kasisi wa Baptist alikuwa mtetezi mashuhuri sana wa mabadiliko ya kijamii kwa njia ya amani. Akitumia kanuni ya bila ya matumizi ya nguvu katika harakati za vuguvugu la haki za kiraia hapa Marekani, Martin Luther King Jr alihubiri usawa wa watu wa rangi zote, wakati ambapo wamarekani weusi walikuwa wahanga wa ubaguzi.

Ujumbe wake wa kuvumiliana ulisaidia kuleta mabadiliko mengine nchini Marekani. Alitoa mojawapo hutuba zinazokumbukwa sana msimu wa joto mwaka 1963 wakati wa maandamano hapa Washington, kuhusiana na ajira na uhuru:
(ACT) …..Ni sharti wakati wote tuendeshe harakati zetu kwa heshima na nidhamu. Kamwe tusiruhusu maandamano yetu kugeuka na kuwa ya ghasia. Tena na tena ni lazima tuinyanyue harakati yetu kukabiliana na mashambulizi ya nguvu kwa kutumia nguvu za nafsi zetu,alisema Dr King.

Martin Kuther King Jr alitoa mwito wa mantiki badala ya chukizo , dhamiri badala ya chuki. Mwaka 1968 aliuawa akiwa mwenye umri wa miaka 39.

Wakati Martin Luther King Jr alifika katika mji mkuu wa Marekani msimu wa joto mwaka 1963, aliwafika kuwatia moyo wamarekani na kuwaraia raia kuzingatia maadili ya waasisi wa taifa letu , alisema rais Bush. Ndoto yake ilisambaza ujumbe wa matumaini, haki na udugu alisema bwana Bush, ambao uliingia katika mioyo ya wanaume kwa wanawake kote katika nchi yetu na unaendelea kuwahimiza mamilioni hapa nyumbani na kote duniani.