Skip Navigation
Skip Left Section Navigation

Kiswahili Editorial

White House on Immigration

January 19, 2007

Rais Bush amesema anataka kushirikiana na bunge la marekani kuandaa mpango mpana wa uhamiaji. bwana Bush amesema anaunga mkono kuongezewa kwa ulinzi katika mipaka na programu ya wafanyi kazi wa muda wakiwa na uwezekano wa hatimaye kuwa raia.

Naamini kwa dhati kuwa twazweza na ni lazima tupate mpango mpana wa uhamiaji. Ni muhimu kwetu sisi kwani ili kutunza usalama kwenye mipaka, ili askari wa kutunza mipaka walioongezewa huko na waliopewa vifaa bora, wanahitaji mpango ili ikiwa unakuja marekani kufanya kazi, uingia kihalali kwa muda, anasema rais Bush.

Msemaji wa ikulu ya white house Tony Snow anasema rais Bush anaelewa uhitaji wa kuwazuiliwa watu kuingia nchini isivyo halali na kuwazuilia wale walioko marekani kufanya kazi isivyo halali.

Anasema ni tatizo kugundua ni nani aliye hapa isivyo halali, watu hawa ni akina nani. Tunahitaji kufahamu. Na kwa hivyo, amezungumza juu ya kitambulishi kisichoweza kufanyiwa ulaghai. Kuna wasi wasi kwamba waajiri huenda wanafahamu kuwa wanawaajiri wageni walioko nchini sivyo halali. katika miaka ya karibuni, utawala huu umezidisha adhabu dhidi ya wale wanaowaajiri wageni wasio halali kutoka faini kwa kosa ndogo haki kuwa adhamu ya jinai na mtu kupokonywa mali zake.

Mfumo wa sasa, anasema rais Bush unawalazimu watu kutafuta kuingia Marekani kwa kuwategemea walanguzi na walaghai, ambao wanawatendea ukatili. Mpango mpana wa uhamiaji, anasema, ni muhimu katika kulinda mipaka ya marekani katika njia ya kiutu.