Skip Navigation
Skip Left Section Navigation

Kiswahili Editorial

US, Colombia Trade Agreement

January 19, 2007

Voice: Mkataba wa kuendeleza biashara wa Marekani na Colombia au CTPA, utaondosha ushuru na vizingiti vingine vya biashara. Mabunge ya marekani na Colombia sharti yaidhinishe mkataba huo kuanza ili uanze kutekelezwa.

Ukiidhinishwa, mkataba wa CTPA utaondosha ushuru katika zaidi ya asilimia themanini ya bidhaa zinazonunuliwa kutoka marekani nchini Colombia. Bidhaa hizo pamoja na zile zakilimo. Mkataba huo kadhalika utaondosha vikwazo dhidi ya makampuni ya huduma yanayofanya biashara nchini Colombia. Pia utatoa utaratibu unaoeleweka wa kisheria kwa wawekezajiw a marekani na kulinda haki ya ubunivu. Mkataba huo utawezesha utekelezaji wa dhati wa sheria za Colombia juu ya ajira na mazingira.

Makamu muakilishi wa biashara wa Marekani John Veroneau alisema mkataba huo ni ishara ya mafanikio makubwa. Makubaliano hayo, anasema yatawanufaisha watumiaji yatapelekea nafasi nyingi za ajira, yatafungua mlango kwa fursa nyingi za kuuza nje bidhaa mpya na kuimarisha uthabiti na usalama kote katika eneo la Amerika kusini.

Tayari bidhaa nyingi za Colombia huingai nchini Marekani bila kutozwa ushuru chini ya mkataba wa biashara wa Andean Trade Preference, ambao utamalizika mwisho wa mwaka.

Waziri wa COlombia wa biashara, viwanda na utalii, Jorge Humberto Botero ameusifu mkataba huo. Mkataba wa biashara huru, anasema utaunda mikondo ya kudumu ili bidhaa zetu zishindane katika soko la marekani, na hivyo kuiletea nchi fedha zaidi na ajira kwa mamilioni ya waColombia.

Mkataba huo anasema makamu muakilishi wa biashara wa marekani Veroneau, utatipa Colombia haki ya kuingia katika soko la marekani kwa wakati wote, hali ambayo itachochea ukuaji, ajira zaidi na kuvutia wawekezaji wapya.