Kiswahili Editorial
Bush on Nato in Afghanistan
January 17, 2007
Alipohudhuria mkutano wa Ushirika wa kujihami wa Atlantic ya Kaskazini NATO huko Riga mji mkuu wa Latvia, rais George Bush alisema, “jukumu msingi la ushirika ni kujihami dhidi ya vitisho vya karne mpya.”
Aliendelea kusema, “tuko katika mapmbano marefu dhidi ya magaidi na wenye siasa kali wa wanaofuata nadhariua ya chuki na kujaribu kubuni himaya ya kiimla kuanzia Hispania hadi Indonesia. Tunapigana dhidi ya wenye siasa kali wanaotafuta mahali penye hifadhi na wako tayari kuwauwa raia wasiyo na hatia kokote kule ili kufikia malengo yao.”
Miaka mitatu iliyopita NATO ilichukua hatua ambayo haijawahi kuchukua ya kupeleka vikosi vyake kulinda utawala wa kidemokrasia uliyo changa huko Afghanistan. Ilikuwa ni mara ya kwanza kabisa kwa NATO kupeleka vikosi vyake njee ya Ulaya. Rais Bush amesema, “tangu kuchukua uwongozi wa kikosi cha kimataifa cha masaada wa usalama huko Afghanistan, NATO imepanua kazi zake kutoka kikosi kidogo kilichokuwa kinafanyakazi huko Kabul pekee na kuwa kikosi thabiti ambacho kinafanya shughuli za usalama katika sehemu zote za Afghanistan.
Aliendelea hueleza kwamba, “NATO ina saidia kutowa mafunzo kwa jeshi la taifa la Afghanistan. Ushirika una timu za kazi za kukarabati nchi katika majimbo ishirini na tano zinazosaidia serekali kuu kupanua uwezo wake wa kufika katika maeneo ya mbali ya nchi. Kwa wakati huu wanachama wote 26 wa NATO na mataifa shirika kumi na moja yanachangia vikosi kwa afisi ya NATO huko Afghnaistan.”
Wapiganaji walobaki wa utawala wa taleban uloondolewa madarakani, magaidi wa al-Qaida, wafanayabiashara haramu wa madawa ya kulevya na mababe wa vita, anasema Rais Bush “ baado wanaendesha shughuli zao na wamenuwiya kuangamiza demokrasia huko Afghnaistan.” Alisema, “ Ili NATO iweze kufanikiwa, makamanda wake ardhini huko wanalazimika kuwa na rasilmali na nafasi wanohitaji kufanya kazi zao. Ushirika ulianzishwa kwa misingi bayana: shambulio dhidi ya mmoja ni shambulio kwa wote. Msingi huo unaukweli ikiwa shambulio linatokea nyumbani kwetu au dhidi ya vikosi vyetu vilivyopelekwa njee kwa kazi ya NATO. Hii leo Afghnaistan ni sehemu moja ambako NATO inaoperesheni muhimu kabisa ya kijeshi na kwa kusimama pamoja na Afghanistan, tutawalinda wananchi wetu, tutalinda uhuru wetu na kupeleka ujumba wazi kwa wenye siasa kali kwamba vikosi vya uhuru na heshima vitashinda.”
Bw Bush amesema kwa sababu ya juhudi za NATO, Afghanistan imepita kutoka enzi ya kikatili ya jinamizi hadi kuwa taifa huru.”




