Kiswahili Editorial
Bush Warns Iran About Iraq
February 14, 2007
Akisema kiwango cha ghasia nchini Iraq hakikubaliki hata kidogo, Rais George W. Bush ametangaza mipango ya kupeleka karibu wanajeshi na marine elfu 20 wa Marekani kuisaidia serikali ya Iraq iliyochaguliwa kidemokrasia kupambana na magaidi na waasi. Ni dhahiri kuwa tunahitaji mabadiliko ya mkakati amesema Bwana Bush.
Kwa kuongezea uboreshaji wa kiwango cha wanajeshi, Bwana Bush alizungumza kuhusu haja ya kutetea hadhi ya Iraq na eneo lake na kuleta uthabiti katika eneo hilo huku ikikabiliwa na changamoto kali.
Hili linaanza kwa kuziangalia Iran na Syria. Tawala hizi mbili zinaruhusu magaidi na waasi kutumia maeneo yao kuingia na kutoka Iraq. Iran imetoa msaada wa vifaa kwa mashambulizi kwa wanajeshi wa Marekani. Tutayavuruga mashambulizi haya kwa majeshi yetu. Tutaingilia kati mtiririko wa misaada kutoka Iran na Syria. Na tutawasaka na kuharibu mitandao inayotoa silaha na mafunzo kwa maadui wetu nchini Iraq anasema Rais Bush.
Bwana Bush amesema kwamba Marekani pia ilikuwa ikichukua hatua nyingine za kuboresha ulinzi wa Iraq na kulinda maslahi ya Marekani katika Mashariki ya Kati.
Hivi karibuni niliamuru upelekaji wa kikosi cha ziada katika eneo hilo. Tutapanua ushirikiano wa habari za kipelelezi na kufanya doria ya anga ya utaratibu wa ulinzi kuwahakikishia usalama marafiki na washirika wetu. Na tutafanya kazi na wengine kuizuia Iran kupata silaha za nyuklia na kutawala katika eneo hilo, anasema Bwana Bush.
Rais Bush anasema kuwa changamoto iliyopo katika Mashariki ya Kati ni kubwa, si mzozo wa kijeshi pekee.
Kwa upande mmoja kuna wale ambao wanaamini uhuru na msimamo wa kadri. Na upande mwingine kuna wale ambao wana msimamo mkali na kutaka kuua watu wasiokuwa na hatia anasema Rais Bush.
Ni kwa maslahi ya Marekani anasema Rais Bush, kusimama pamoja na wanaume na wanawake jasiri ambao wameyatoa maisha yao ili kudai uhuru, na kuwasaidia wakati wakifanya kazi ya kuwa na jamii zenye usawa katika Mashariki ya Kati.




