Kiswahili Editorial
Stopping Iran’s Nuclear Menace
February 26, 2007
Utafutaji wa silaha za nuklia unaofanywa na serikali ya Iran unatishia majirani wa nchi hiyo na dunia nzima kwa jumla, anasema Gregory Schulte, Balozi wa Marekani katika Idara ya Kimataifa ya Nguvu za Atomiki. “Hata bila ya kutumia silaha moja ya nuklia,” alisema Bw Schulte, “hali tu ya kuwa na silaha za nuklia inaweza kutia nguvu viongozi wa Iran kutumia majeshi yao ya kawaida na kuongeza juhudi za ugaidi kuendeleza mipango yao katika eneo.”
Katika hotuba iliyotolewa Munich, Ujerumani, Bw Schulte alisema ni muhimu kuwa Ulaya na Marekani zinashirikiana kwa kutumia diplomasia imara kuizuia Iran kupata silaha za nuklia. “Kampeni ambayo si ya kijeshi, kama ikiwa ya nguvu na ya muda mrefu, na ikiungwa mkono na nchi nyingine,” anasema Bw Schulte, “ ina uwezekano wa kufanikiwa dhidi ya utawala ambao umeshindwa kutekeleza ahadi zake za kiuchumi, ambao unahitaji uwezekaji wa nje kwa mapato ya serikali, na ambayo inakabiliwa na upinzani mkubwa ndani ya nchi.”
Bw Schulte amesifu “hatua za haraka” za Umoja wa Ulaya katika kutekeleza azimio namba 17-37 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Azimio hilo linaamrisha nchi zote wanachama kuwacha kuipa Iran vifaa au teknolojia ambayo inaweza kusaidia mpango wa nuklia au mizinga ya masafa marefu. Lakini, anasema Bw Schulte, “Umoja wa Ulaya na nchi za Ulaya zinaweza kufanya mengi zaidi kuongeza nguvu juhudi za kidiplomasia...Ulaya haina budi kutumia hatua zote zisizo za kijeshi ilizo nazo. Kwa nini, kwa mfano, anasema Bw Schulte, “serikali za Ulaya hazichukuia hatua zaidi kuzuia uwekezaji na shughuli za kifedha.”
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Sean McComark anasema baadhi ya serikali za Ulaya zina wasiwasi kuhusu “masharti ya kisheria” katika swala hilo. Lakini, anasema, kumekuwa na maendeleo katika sekta ya binafsi.
”Unaona nchi za Ulaya pamoja na biashara nyingine binafsi zikifanya maamuzi ya kibiashara kutokana na wasiwasi wa kifedha au sifa zao endapo watawezekeza Iran, nchi ambayo sasa iko chini ya maazimio ya Umoja wa Mataifa.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, McComark, anasema Marekani itaendelea kushirikiana na nchi nyingine kuweka shinikizo dhidi ya Iran. “Hilo halina budi kutazamiwa kutokana na ukubwa wa swala hili. Iran kupata silaha za nuklia,” anasema McComark. “Hakuna anayetaka hilo.”




