Kiswahili Editorial
Iranian Women Working For Change
March 5, 2007
Nchini Iran, kampeni inaendelea ya kukusanya sahihi kudai mabadiliko ya sheria ambazo zinawabagua wanawake. Wanawake elfu 30 wa Iran wameripotiwa kuweka saini zao hadi sasa.
Hivi sasa, wanawake nchini Iran wamepewa haki chache mno kwa mujibu wa sheria kuliko wanaume katika masuala ya talaka, ulezi wa watoto na urithi. Kwa kuongezea, ushahidi wa mwanamke katika mahakama za Iran una thamani ndogo mno kuliko wa mwanamme. Wanawake wanazuiliwa kusafiri bila ya idhini ya mume au jamaa wa kiume. Wasichana wadogo wenye umri wa miaka tisa tu wanaweza kuolewa. Kuuawa kwa kunyongwa au kurushiwa mawe kwa vitendo vya ngono ni adhabu inayokubalika kisheria na kuadhibiwa wanawake.
Kampeni ya kukusanya sahihi kuhusu madai ya mabadiliko hayo ulianza August mwaka 2006. Lengo ni kukusanya sahihi milioni moja katika muda wa miaka miwili na kuwasilisha madai kwa bunge la Iran kwa ajili ya kuchukua hatua za marebekisho ya kisheria. Msukumo wa kampeni hii ulianzishwa na kundi la taasisi za wanawake nchini Iran baada ya majeshi ya usalama kuvunja kwa kutumia nguvu maandamano ya amani ya kudai haki yaliyofanyika mjini Tehran mwezi June mwaka 2006, na kuwapiga na kuwakamata dazeni ya watu.
Katika kampeni ya kudai haki, wanawake nchini Iran wanagawa vikaratasi kwa wanawake wengine wa iran kuwaelezea kuhusu sheria za sasa. Wanakampeni pia wamefungua mtandao. Juhudi za kuanzia ngazi za chini, kampeni ina uungaji mkono wa wanawake maarufu nchini Iran, kama vile mshindi wa tuzo ya amani, Shirin Ebadi na mwandishi maarufu wa mashairi, Simin Behbahani.
Lakini wakati maandamano ya amani ya kudadi haki nchini Iran yakithibitika kuwa ni hatari, na ushiriki wa kampeni katika kampeni nao pia ni hivyo hivyo. Hivi karibuni, waandishi wa habari watatu wa kike ambao walikuwa wakijishughulisha sana na kampeni hii walikamatwa na kuhojiwa kwenye gereza la Evin. Tala’t Taghinia, Mansoureh Shojaie na Farnaz Seify walipekuliwa nyumba zao, kompyuta zao na nyaraka ziliibiwa, na hivi sasa wanakabiliwa na kesi mashtaka na Serikali ya Iran. Washiriki wengine pia wamekamatwa, wamepoteza kazi zao, simu zao zinasikilizwa, na kuzuiliwa kusafiri nje ya nchi.
Rais George W. Bush amesema kwamba vitendo na ushiriki kamili wa wanawake ni muhimu sana katika mafanikio ya jamii yoyote.
Kwa vile wanawake wamekuwa sehemu ya utaratibu wa demokrasia, wanaweza kusaidia katika kusambaza uhuru na haki, na lililo muhimu kuliko yote ni matumaini ya hali ya baadae anasema.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Sean Mccormack akiongea kuhusu ukandamizaji wa wanawake, pamoja na makundi mengine, kunakofanywa na Serikali ya Iran, amesema, Marekani inautaka utawala wa Iran kuacha kuwakandamiza raia wake, na kuheshimu haki za binadamua na watu wote wa Iran.




