Kiswahili Editorial
Liberian Debt
March 5, 2007
Marekani imetangaza kwamba itafuta karibu deni la dola bilioni nne ambalo Liberia inadaiwa. Akiongea katika mkutano wa Liberia Partner;s Forum hapa Washington, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Condoleezza Rice alizungumzia ahueni ya deni kama sehemu ya nia ya dhati ya Marekani katika ujenzi na maendeleo nchini Liberia.
Tutafuta deni hilo, lote, kwa mujibu wa muundo wa nchi ambazo zina madeni makubwa. Tuna matumaini kwamba hii itasaidia kuipa ahueni Liberia ambayo inadumuzwa na mzigo wa madeni, mzigo wa deni ambalo viongozi wa leo na waliberia wa leo hawastahili kulibeba. Tuna matumaini kwamba itaiwezesha serikali kuelekeza rasimali zake moja kwa moja katika ujenzi na maendeleo, anasema Bi Rice.
Baada ya karibu miaka 14 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na vifo karibu laki mbili na nusu, Bi Rice amesema, ni wakati wa matumaini nchini Liberia. Wakimbizi wanarejea kwenye nchi yao na waliberia wanajenga tena jamii zao. Uwekezaji wa uchumi, ukuaji na ufufuaji unaanza kuchukua mwelekeo mpya. Kwa mfano, shirika la Kimataifa la Fedha Duniani limeripoti kwamba mwaka 2006, kiwango cha mapato ya ndani ya mwaka cha Liberia kilipanga na kukadiriwa kufikia asilimia saba na nusu kutoka asilimia tano na nusu mwaka 2005.
Rais Ellen Johnson Sirleaf, ambaye alichaguliwa kushika wadhifa wa urais mwaka 2005, amekiri kwamba amani nchini Liberia bado ni tete mno kuliko miaka mitatu baada ya rais wa zamani Charles Taylor kulazimishwa kuondoka madarakani. Kuimarisha amani na ulinzi, Bi Sirleaf amesema limekuwa ni jukumu lake la juu.
Katika juhudi ya kuisaidia Liberia kuijenga tena, Marekani imetoa dola milioni 500 msaada wa ahueni na maendeleo tangu mwaka 2003. Maendeleo ya kudumu ya uchumi yanahitaji sekta binafsi ambazo ni madhubuti, biashara huru, na fursa ya kufika katika masoko ya kimataifa. Kwa hilo, shirika la Marekani la kimataifa la Uwezekaji katika sekta binafsi linafanya kazi na biashara kuboresha mtaji kwa wafanyabiashara wa Liberia na pia wafanyabiashara ndogo ndogo.
Marekani ina nia ya dhati kuisaidia Liberia kujibadili yenyewe na kuwa nchi yenye mafanikio na amani. Haya ni malengo mazuri sana ambayo watu wa Liberia wamejiwekea wenyewe, amesema Waziri wa Mambo ya Nje Rice na ni katika mwelekeo huo kwamba wao na viongozi wao wa kidemokrasia wanashinda. Wanahitaji na kustahili msaada wetu.




