Kiswahili Editorial
Expanding US-India Trade
March 8, 2007
Waziri mdogo wa maswala ya uwekezaji, katika wizara ya marekani ya fedha, Timothy Adams anasema, nanukuu, “ India inakuwa na na ushiriki mkubwa katika biashara na uwekezaji duniani, na uhusiano wa kiuchumi baina ya marekani na India, umeimarika. Mauzo ya bidhaa za Marekani kwenda India ya kila mwaka, yameongezeka mara mbili tangu mwaka 2000, anasema Adam nao ununuzi wa bidhaa za India hapa Marekani, umeongezeka kwa asilimia saba. Thamani ya uwekezaji wa moja kwa moja wa wamarekani nchini India umeongezeka zaidi ya maradufu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, kutoka dola bilioni mbili na milioni mia mbili mwaka 2000 hadi kufikia dola bilioni nane nukta tano mwaka 2005.
Watu wa India wananufaika kutokana na upanuzi huo wa biashara. Pato jumla la India limekuwa hadi kuzidi asilimia tisa. Kiwango cha umasikini katika nchi hiyo kimepungua kutoka takriban asilimia arubainnne hadi chini ya asilimia thelathini katika kipindi cha miaka kumi. Kiwango cha watu wazima wanaojua kusoma na watoto wanaomaliza shule ya msingi, kimeongezeka. Na teknolojia inaendelea kupatikana kwa urahisi, ikiwa ni pamoja na ongezeko la mara kumi na nne katika matumizi ya simu za mkononi, katika kipindi cha miaka minne iliyopita.
Bwana Adam anasema ukuaji imara wa India haungewezekana bil aya sera za serikali za kufungua masoko ya nchi hiyo, yakabiliwe na ushindani. Mageuzi ya kiuchumi ya India yalianza mapema miaka ya 1990 wakati Manmohan Singh , ambaye sasa ni waziri mkuu wa India alikuwa waziri wa fedha. India ilipunguza ushuru wa bidhaa za kibiashara, ukalegeza vikwazo dhidi ya bidhaa ambazo hazitozwi ushuru, ikaondoa vikwazo dhidi ya utoaji leseni wa bidhaa vinavyotumika kutengenezea vifaa mbali mbali. Matokeo yake ni kwamba biashara jumla ya India imekuwa kutoka chini ya asilimia kumi na tano hadi kufikia asilimia arubainne.
Waziri mdogo wa fedha Adamas anasema India imechukuwa hatua kulegeza udhibiti katika uwekezaji wa kigeni pamoja na mikopo. Mageuzi hayo anasema Adams, yameiletea India mafanikio makubwa katika uchumi wa kimataifa. Lakini utandawazi pia umewasilisha changamoto mpya. Ili kukamilisha mageuzi katika kuufanya uchumi wake wa kisasa kabisa, India inahitaji kupunguza vikwazo dhidi ya kibiashara na uwekezaji na kuruhusu uhuru zaidi katika sekta yake ya fedha pamoja na kuboresha mazingira yake ya kufanyia biashara.
Waziri mdogo Timothy Adams anasema India yahitaji kulishinda shinikizo linaloathiri kila uchumi na kuboresha mazingira ya uwekezaji. Ikifaulu anasema, usoni wake utakuwa wenye mafanikio makubwa.




