Kiswahili Editorial
Reducing Dependence on Oil
February 14, 2007
Rais George W. Bush anasema kwamba moja ya changamoto kubwa zinazoikabili Marekani ni kubuni njia za kupunguza utegemezi katika mafuta hasa mafuta kutoka nje. Utegemezi kama huo, amesema, unaifanya Marekani iwe katika hali hali isiyo ya usalama na serikali ambazo si rafiki.
Kwa maneno mengine, kuna mtu hatupendi, wanazalisha mafuta, wanaamua kufanya kituo kuhusu hayo mafuta, wanaweza kutuathiri…. Hutaki Rais wako akae tu ofisini kwenye Ikulu ya White House awe na wasi wasi kuhusu harakati za tawala dhalimu ambazo zina mshtuko wa kila aina kwa usalama wetu, kuanzia kwenye usalama wa uchumi anasema Bwana Bush.
Utegemezi kwa mafuta ya nje, amesema Bwana Bush, pia unaifanya Marekani iwe katika hatari kwa magaidi.
Kama magaidi wangekuwa na uwezo wa kuharibu miundo mbinu kwingineko duniani, pia itaathiri kwa kile tutakacholipia kwa mafuta. Magaidi wametushambulia kwa njia ambazo ni za kikatili mno; walitushambulia kwa kutumia ndege na kuvamia majengo yetu. Lakini pia tuko katika hatari ya mashambulizi kupitia miundo mbinu kote duniani ambayo yanaweza kusababisha bei kupanda sana, anasema Rais Bush.
Ili kupunguza hatari hii kwa Marekani kwa hali ya ugavi mafuta hapo baadae, Wizara ya Nishati ya Marekani haraka itaanza kuongeza maradufu akiba ya mafuta katika ghala ya akiba ya mafuta ambayo ni kwa ajili ya matumizi ya dharura ya Marekani, na kufikisha mampia bilioni moja na nusu ifikapo mwaka 2027. Marekani tayari imeongeza akiba yake kwa mapipa milioni 100 na hivi sasa ina kiwango cha mapipa milioni 700.
Rais Bush amelitaka Bunge la Marekani kuunga mkono upanuzi wa ugavi mbadala wa mafuta kama vile ethanol, mafuta ambayo yatatengenezwa kwa kutumia usindikiaji na uchujaji wa mahindi. Pia ametaka zitengenezwe gari ambazo zitatumia mafuta kwa kiasikidogo, na hivyo kuokoa mabilioni ya galoni za mafuta katika kipindi cha miaka kumi ijayo.
Kwa kuchukua hatua hizi, amesema Rais Bush tunaweza kusaidia kufanikisha lengo kubwa: kupunguza matumizi ya mafuta hapa Marekani kwa asilimia 20 katika kipindi cha miaka kumi ijayo na kupunguza ununuzi wetu wa jumla wa mafuta kutoka nje kwa robo tatu ya mafuta yote ambayo hivi sasa tunanunua kutoka Mashariki ya Kati.




