Speeches
IKULU YA WHITE HOUSE
Ofisi ya Katibu wa Mitambo
Julai 11, 2009
HOTUBA YA RAIS BARACK OBAMA
NGOME YA CAPE COAST
Ngome ya Cape Coast
Cape Coast, Ghana
Saa kumi kasoro dakika tatu, Saa za Greenwich (GMT)
RAIS: Michelle, watoto na vile vile jamaa zangu wengine, tumepewa matembezi ya kipekee katika ngome hii. Inanikumbusha ziara niliyofanya Buchenwald kwa sababu inatukumbusha uwezo wa binadamu kufanya maovu makubwa. Mojawapo ya vitu vya ajabu sana nilivyosikia ni kwamba juu ya mashimo ambamo watumwa wa kiume walishikiliwa kulikuwa na kanisa, na hili linatukumbusha kwamba mara nyingine tunaweza kuvumilia na kutetea uovu mkubwa hata kama tunafikiri kuwa tunafanya mambo mazuri.
Unajua, ninafikiri ilikuwa muhimu hasa kwa Malia na Sasha, ambao wanakulia katika hali ya kubarikiwa sana, kukumbushwa kwamba historia inaweza kuchukua mkondo wa ukatili mkubwa, na tunatumaini kwamba kitu kimoja walichopashwa wakati wa ziara hii ni hisi ya wajibu wao wa kupambana na ukandamizaji na ukatili popote pale unapotokea, na kwamba kundi lolote la watu ambao hawajali kundi jingine la watu lazima tupambane nao kwa kutumia vifaa vyovyote tulivyo navyo.
Kwa hiyo waziwazi, ni tukio la hisia kubwa, muda wa hisia kubwa. Tunataka kuwashukuru wale waliopanga matembezi haya na kwa watu wa Ghana kwa kuhifadhi historia hii. Ingawa ni jambo la uchungu, ninafikiri inasaidia kutufundisha sote kwamba tunalazimika kufanya kila tunaloweza kupambana na aina ya uovu ambao, kwa kusikitisha, bado upo katika ulimwengu wetu, na si katika bara hili peke yake lakini katika kila pembe ya dunia hii.
Na ninafikiri, kama Wamerikani, na Wamarekani wenye asili ya Kiafrika, ni dhahiri kuna hisia maalumu kwamba kwa upande mmoja hapa palikuwa eneo la majonzi makubwa; kwa upande mwingine, ni hapa ambapo ziara ya uzoefu wa wengi kati ya Wamarekani wenye asili ya Kiafrika ilipoanzia. Na kama ishara, kuweza kurudi na familia yangu, nikiwa na Michelle na watoto wetu, na kuona lango ambalo walipitia wale walioanzisha ulimwengu mpya, lakini vile vile kuweza kurudi hapa kusherehekea pamoja na watu wa Ghana maendeleo ya ajabu ambayo tumeyafanya kwa sababu ya ujasiri wa wengi, weusi kwa weupe, kutokomeza utumwa na hatimaye kupata haki za kiraia kwa watu wote, ninafikiri ni chanzo cha matumaini. Inatukumbusha kwamba ingawa historia inaweza kuwa mbaya, inawezekana pia kushinda.
Asanteni, kila mtu.
MWISHO - saa kumi zaa za Greenwich (GMT)




