Skip Navigation
Skip Left Section Navigation

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari

Kikundi cha muziki wa jazz kutoka Marekani chatua Dar-es-Salaam Jumanne

  • Tamasha la bure Chuo Kikuu Dar na Ngome Kongwe
  • Warsha kwa wanafunzi wa muziki na wanamuziki wengine Dar & Zanzibar
  • Januari 31, 2006

    Kikundi cha wanamuziki mashuhuri wa jazz kutoka Marekani kinawasili Dar-es-Salaam leo mchana kwa ziara ya maonyesho ya siku nne nchini Tanzania. Kikundi hicho kinachojulikana kama: The Annette Aguilar and Stringbeans Latin Jazz Quartet kitafanya maonyesho jijini Dar-es-Salaam na Zanzibar.

    Baada tu ya kuwasili, wanamuziki hao watafanya mahojiano na vituo vikubwa vya redio jijini Dar-es-Salaam. Jumatano jioni watafanya tamasha la bure kwenye Ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam wakisindikizwa na kikundi cha hapa nchini InAfrika Band.

    Kwa mujibu wa taarifa ya Ubalozi wa Marekani, ziara hii imefadhiliwa na Ubalozi pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani na mpango wa Jazz at Lincoln Center: American Music Abroad program. Wanamuziki wanaoshiriki katika ziara hiyo ni Annette A. Aguilar (percussion), Freddie Bryant (guitar), Rob Thomas (violin and bass), na Barry Olsen (keyboard, trombone, percussion and vocal). Annette, Rob na Barry walikuwa kwenye kikundi cha Jazz Ambassadors ambacho kilitembelea Afrika ya Kusini, Botswana, Swaziland, Namibia na Rwanda mwaka wa 2003. Freddie Bryant na kikundi chake walizuru nchi za Asia ya Mashariki na Kusini mwaka 2003 na Februari 2005, Bryant peke yake alikuja Dar es Salaam, Zanzibar na Nairobi.

    Ziara yao ya hivi sasa itawapeleka Madagascar, Ethiopia, Tanzania na Kenya, na itawapa fursa ya kuwapa wanamuziki wengine ujuzi wao wa muziki wa Marekani na Visiwa vya Caribbean. Kikundi hiki mahiri kinapiga midundo murua ya Afro-Cuban, Jazz na Afro-Brazilian kwa kutumia guitar, violin, trombone piano na bass.

    Kikundi hicho kitakuwa Zanzibar Jumamosi Februari 4, 2006 na kufanya warsha kwa wanafunzi wa muziki na wanamuziki wengine kwenye chuo cha Dhow Countries Music Academy (DCMA). Baadaye jioni, bendi hiyo itatumbuiza pamoja na InAfrika Band kwenye Ngome Kongwe (Old Fort). Kiingilio ni bure.

    Bendi hiyo itaondoka nchini Jumapili Februari 5, 2006 kuelekea Nairobi, Kenya ambako watafanya ziara kama hiyo.

    - Translation -
    This content is also available in English