Skip Navigation
Skip Left Section Navigation

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari

Ubalozi wa Marekani wafadhili shindano la kazi za sanaa kama sehemu ya kuadhimisha Siku ya Mazingira

  • Mshindi kupata tuzo ya dola 1,000 au nafasi ya kutembelea Marekani
  • Machi 20, 2007

    Katika kuadhimisha miaka 37 ya Siku ya Mazingira hapo Jumapili Aprili 22, 2007, Ubalozi wa Marekani jijini Dar-es-Salaam unafadhili shindano la kitaifa la kazi za sanaa za vijana wa Kitanzania. Kaulimbiu ya shindano hilo ni: “Kitu gani kwako ni muhimu kuhusu mazingira yetu?”

    Washindani watawekwa kwenye makundi matatu kulingana na umri wao. Kundi la kwanza ni la vijana wenye umri wa miaka 10-11; la pili, miaka 12-13; na la tatu, miaka 14-15. Washindi watatu watachaguliwa kutoka kila kundi na majina yao yatawasilishwa kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani mjini Washington D.C., ili kushindania zawadi ya kwanza itakayotolewa kwa mshindi wa kimataifa katika kila kundi. Zawadi hiyo ya kimataifa itakuwa ni kiasi cha fedha kinacholingana na dola 1,000 au safari ya kutembelea Marekani.

    Kazi ya sanaa itakayowasilishwa inaweza kuwa ya aina yoyote, alimradi inaweza kupigwa picha na kupelekwa Washington. Mwisho wa kuwasilisha kazi hizo za sanaa ni Jumatatu, Aprili 2, 2007. Uamuzi utafanyika Aprili 3 na washindi watatangazwa Siku ya Mazingira, Aprili 12, au baadaye kidogo. Katika mwezi mzima wa Aprili, Ubalozi wa Marekani utaonesha baadhi ya kazi za sanaa zitakazoingia kwenye shindano hilo. Kazi za sanaa zitazowasilishwa kwenye shindano hilo hazitarudishwa kwa wenyewe.

    Washindani wanatakiwa kuwasilisha kazi zao za sanaa kwenye lango kuu la Ubalozi wa Marekani ulio Barabara ya zamani ya Bagamoyo, Msasani, wakati wa saa za kazi (Jumatatu-Alhamisi: saa 1:30 asubuhi – saa 11:00 jioni; Ijumaa saa 1:30 asubuhi – saa 5:30 asubuhi). Kazi hizo za sanaa zifungashwe vizuri na kuandikwa juu yake “Attention Public Affairs Office,” zikiambatana na taarifa kuhusu jina kamili la msanii, umri wake, tarehe ya kuzaliwa, anwani yake, pamoja na maelezo mafupi kuhusu kazi hiyo, na kitu gani ni muhimu kwa mshindani kuhusu mazingira. Kazi za sanaa zitakazowasilishwa baada ya saa 11:00 jioni, Jumatatu Aprili 2, 2007 hazitashughulikiwa.