Skip Navigation
You Are In: Home > Habari Kutoka Ubalozi > Kiswahili Press Releases > Mkutano Kati ya Marais Barack Obama na Jakaya Kikwete
Skip Left Section Navigation

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari

Close Window Rais Barack Obama akizungumza na  Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete katika ofisi yake - Ikulu, Washington DC Marekani, hapo tarehe 21 Mei 2009.
Rais Barack Obama akizungumza na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete katika ofisi yake - Ikulu, Washington DC Marekani, hapo tarehe 21 Mei 2009.

Mkutano Kati ya Marais Barack Obama na Jakaya Kikwete

May 22, 2009

Rais Barack Obama na Rais Jakaya Mrisho Kikwete walikutana adhuhuri Mei 21 na kuwa na majadiliano muhimu kuhusu masuala mbalimbali. Rais Obama alielezea kufurahishwa kwake kutokana na ushirikiano mzuri na wa karibu uliopo baina ya Marekani na Tanzania. Aidha, Marais hao walibadilishana mawazo kuhusu mbinu mbalimbali za kuboresha ubia ulipo kati ya Marekani na Tanzania na kuboresha sera za maendeleo katika nyanja za afya, elimu na kilimo. Hali kadhalika walijadiliana kuhusu namna ya kufanya kazi na wadau wengine katika kanda ili kutatua baadhi ya migogoro mikubwa katika bara la Afrika. Marais Obama na Kikwete walielezea azma ya kuendelea kufanya kazi pamoja ili kutatua matatizo ya pamoja katika siku zijazo. Rais Kikwete ni Rais wa kwanza kutoka Afika kumtembelea Rais Obama katika Ikulu ya White House.