| - Translation - |
| This content is also available in English |
Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
Ofisa wa Marekani atua Dar kujadili mkataba wa kuzuia silaha za nyuklia
June 22, 2006
Naibu Waziri Kiongozi wa Kitengo cha Uchunguzi, Usimamizi na Ukaguzi wa nyuklia katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Dk. Christopher Ford alitembelea Tanzania wiki hii kujadiliana na viongozi wa serikali ya Tanzania umuhimu wa mikataba na makubaliano ya kimataifa juu ya kuzuia ueneaji, usimamizi na uchambuzi wa silaha za nyuklia.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani, Dk. Ford alikutana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Profesa Juma Kapuya, Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula na maofisa wa ngazi za juu wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia na Elimu ya Juu. Katika mkutano wao walijadili nafasi ya mabadilishano ya mawazo na uhusiano kati ya Marekani na Tanzania kuhusiana na maafikiano yanayohusu mkataba wa kuzuia ueneaji wa silaha za nyuklia na maafikiano ya ulinzi kama yalivyoainishwa na Taasisi ya Kimataifa ya Nguvu za Atomiki, Mkataba wa Silaha za Madawa na ule uhusuo Silaha za Kibaolojia.
“Tanzania kama mjumbe mwenye kura katika Baraza la Usalama na mjumbe wa kimataifa ina nafasi muhimu ya kushugulikia masuala haya, taarifa ilieleza,” na kuongeza kuwa ziara ya Dk. Ford si tu ya kuitumainisha Tanzania kuendelea kutekeleza majukumu yake kufuatana na Makubaliano ya Mkataba bali pia ni kuimarisha uwezo wa Tanzania wa kuthamini utekelezaji wa nchi nyingine.
Wakati dunia inahangaishwa na uwezekano wa Korea ya Kaskazini wa kuanzisha ‘missile’ na azma ya Iran ya kuendeleza nyuklia hata kama hili ni kwa gharama ya Mkataba wake, masuala yahusuyo kuzuia ueneaji, usimamizi na uchambuzi wa Mkataba na maafikiano ya kimataifa ya silaha ni muhimu sana, taarifa hiyo ilieleza.
Korea ya Kaskazini na Iran ni mifano ya upuuzwaji wa Kimataifa. Jumuia ya Kimataifa inahitaji kwa sauti moja kwa kupitia Umoja wa Mataifa na vyombo vingine vya kimataifa kusisitiza kuwa mataifa yote ni lazima yatekeleze majukumu ya Mkataba ambayo wameyaridhia kwa hiari yao na kuyafanyia kazi ili kuzuia wengine wenye dhamira za kukiuka mkataba huo.
Mashauriano ya Dk. Ford hapa Dar es Salaam ni sehemu ya ziara yake ya nchi nne kuonana na maofisa wa ngazi za juu wa Afrika nchini Tanzania, Afrika ya Kusini na Gambia.



