Skip Navigation
You Are In: Home > Habari Kutoka Ubalozi > Kiswahili Press Releases > Jiunge Na Ukurasa Wa Facebook Wa Ubalozi Wa Marekani
Skip Left Section Navigation

Habari Kutoka Ubalozi

Close Window Ukurasa Wa Facebook Wa Ubalozi Wa Marekani, Tanzania
Ukurasa Wa Facebook Wa Ubalozi Wa Marekani, Tanzania

Jiunge Na Ukurasa Wa Facebook Wa Ubalozi Wa Marekani

Hivi sasa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania upo katika Mtandao wa Facebook, kuwa Mpenzi wa Facebook hiyo ili upate taarifa mpya mbalimbali

15 Julai 2009

Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umejiunga na mageuzi ya Mtandao wa Web 2.0 kwa kuzindua ukurasa wake wa Facebook. Balozi nyingi za Marekani duniani zinatumia Facebook kama njia ya kuwezesha mawasiliano ya moja kwa moja kati ya balozi hizo na umma kuhusu mada mbalimbali kama vile Sera ya Mambo ya Nje ya Marekani na shughuli za Ubalozi. Kwa kuzinduliwa kwa ukurasa huu wa Facebook, Watanzania wana jukwaa ambalo wanaweza kulitumia kutoa michango yao ya mawazo na hata kujadiliana kuhusu masuala mbalimbali yanayouhusu Ubalozi.

Unaweza kupata ukurasa wa Facebook wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, kwa kutafuta (search) “Embassy Tanzania” katika mtandao wa Facebook, au kwa kuingia moja kwa moja kwa kutumia anuani ifuatayo:

http://www.facebook.com/tanzania.usembassy

Hivi sasa ukurasa huo una taarifa mbalimbali kuhusu ziara ya Rais Barak Obama huko Ghana, ikiwa ni pamoja hotuba yake kamili ikiwa imetafsiriwa katika Kiswahili. Mara kwa mara, ukurasa huu utakuwa ukiboreshwa na kuwekwa taarifa mpya zinazowagusa Watanzania. Watumiaji wote wa Facebook nchini Tanzania na duniani kote wanakaribishwa kutembelea ukurasa huu wa na kushiriki katika majadiliano kwa njia ya mtandao.

Aidha, watumiaji wa mtandao ambao tayari wa akaunti za Facebook wanakaribishwa kuwa Wapenzi (Fans) wa Ukurasa wa Facebook wa Ubalozi wa Marekani Tanzania kwa kubofya mahali palipoandikwa “Become a Fan” ili uweze kuwasiliana na wapenzi wengine wa ukurasa huo na kupata taarifa mpya kutoka Ubalozini!

 
Article translated in: