Hotuba
Uzinduzi wa Shule ya Msingi Tongoni
Jumatano, 29 Julai 2009
Hotuba ya Kaimu Balozi Larry André (Kama ilivyotayarishwa)
Waheshimiwa wageni waalikwa.
Mheshimiwa Said Kalembo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Dr. Ibrahim Msengi, Mkuu wa Wilaya ya Tanga
Mstahiki Meya, Kassim Kisauji
Wananchi wa Kijiji cha Tongoni
Mabibi na mabwana.
Asubuhi ya leo tunasherehekea kukamika kwa kazi ya ukarabati wa majengo ya shule hapa Tongoni. Kazi hii imefanikiwa kutokana na ubia kati ya Jeshi la Marekani na Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Ubia wetu huu ulipata mwogozo mzuri kutoka kwa uongozi wa Mkoa wa Tanga na msaada mkubwa kutoka kwa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) na kufadhiliwa na watu wa Marekani. Tunaongozwa na Rais Obama na Rais Kikwete, ambao wote wamesisitizia suala la kuwapa elimu watoto kama uwekezaji ambao hatimaye utawezesha maisha bora kwa wote.
Kazi ambayo sisi na wabia wetu tumeifanya itawasaidia zaidi ya watoto 500 kutoka vijiji mbalimbali wanaopata masomo yao katika shule hii. Kazi yote hii ya ukarabati, --paa na msingi wa madarasa, milango na madirisha – ikijumuishwa na dhamira ya dhati ya viongozi wa Mkoa wa Tanga katika kuboresha elimu, itawawezesha watoto hawa kusoma na kujifunza zaidi. Kwa kadri watoto hawa watakavyokuwa wakikua, ndivyo elimu yao itawapa fursa nyingi zaidi za kuwa na maisha bora na hivyo kuboresha hali ya hapa Tongoni na vijiji jirani. Haya ndio maendeleo.
Ninawapongeza, walimu, viongozi wa kiserikali na viongozi wa jamii ambao kwa pamoja wamefanya kazi kubwa katika kuwezesha ukarabati huu, Ninawatakia nyote, hususan, wanafunzi, mafanikio makubwa katika jitihada za kuboresha maisha yenu, maisha ya jamii zenu na hatimaye kuinua taifa lenu!
Asanteni Sana!




