Skip Navigation
Skip Left Section Navigation

Taarifa kwa vyombo vya habari

USAID yatoa $3.1 milioni kuboresha afya za familia za Watanzania

Agosti 24, 2005


Shirika la Misaada la Marekani (USAID) na Wizara ya Fedha ya Tanzania, jana Agosti 23, 2005 zimetiliana saini mkataba wa $3,164,068 kusaidia maendeleo katika sekta ya afya Tanzania, na inatoa nyongeza ya $9 milioni za msaada kwa ajili ya shughuli za afya kupitia vyombo mbalimbali. Msaada huuo utatumiwa na Serikali ya Tanzania katika kuboresha hali ya afya ya familia za Watanzania.

Msaada huo wa fedha na vifaa unaotolewa na USAID utawezesha kuboresha huduma za uzazi, afya ya mama na mtoto, ikiwemo maongezo ya vitamini A, uzazi wa mpango, udhibiti wa malaria na kaswende kwa kinamama wajawazito, na kulinda mimba changa zisiweze kuharibika. Shughuli hizo pia zitaimarisha sekta ya afya iliyo bora na kutoa madaraka ya mfumo wa afya katika ngazi za wilaya.

Mwaka jana USAID ilitoa takribani dola za kimarekani milioni 13 kwa Tanzania katika sekta ya afya na programu za maendeleo. Chini ya makubaliano mapya yaliyosainiwa, USAID itaendelea na mpango wake wa kusaidia sekta ya afya kwa ushirikiano wa karibu na Wizara ya Afya. Vilevile, mipango mbalimbali itaendelea kwa ajili ya kuimarisha maendeleao ya afya yaliyopo kwa kuhamasisha wilaya na jamii kuendeleza ushirikiano wa sekta binafsi na za umma, kukiwepo huduma za sekta zote za kujitolea, binafsi na za umma. Na zaidi ya kuimarisha uwezo wa huduma bora, USAID itasaidia kuhamasisha uhitaji wa uzazi bora wa mpango na huduma za afya kwa mama na mtoto.

Utafiti wa afya uliofanywa unaonyesha kwamba kumekuwa na kushuka kwa idadi ya vifo kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano (takribani asilimia 25 katika kipindi cha miaka mitano iliyopita). Wakati habari hizo ni njema, bado kiwango cha vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano ni kikubwa, na kinatakiwa kushuka zaidi.

Utafiti huo pia unaonyesha kwamba kiwango cha vifo vya wajawazito havijabadilika katika kipindi cha miaka mitano, na kuna uhitaji mkubwa sana wa huduma za uzazi wa mpango. Msaada unaotolewa na USAID utasaidia Serikali ya Tanzania kuzungumzia masuala hayo muhimu ambayo yanaathiri afya za familia za kitanzania.

- Translation -
This content is also available in English