Skip Navigation
You Are In: Home > Habari Kutoka Ubalozi > Kiswahili Press Releases > Waandishi wa Habari Wapatiwa Mafunzo nchini Marekani
Skip Left Section Navigation

Press Release

Close Window Waandishi wa habari wa Kitanzania kutoka vyombo mbalimbali vya habari waliorejea nchini hivi karibuni kutoka nchini Marekani walipokuwa wakishiriki programu maalumu ya mafunzo ya mwezi mmoja kwa ufadhili wa watu wa Marekani
Waandishi wa habari wa Kitanzania kutoka vyombo mbalimbali vya habari waliorejea nchini hivi karibuni kutoka nchini Marekani walipokuwa wakishiriki programu maalumu ya mafunzo ya mwezi mmoja kwa ufadhili wa watu wa Marekani

Waandishi wa Habari Wapatiwa Mafunzo nchini Marekani

25 Agosti 2009

Waandishi wa habari tisa kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wamerejea nchini hivi karibuni baada ya kuhudhuri programu ya mafunzo ya mwezi mmoja nchini Marekani kwa ufadhili wa watu wa Marekani kwa kupitia Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).

Programu hiyo iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Maine nchini Marekani ililenga katika mbinu mpya za uandishi wa taarifa za uchunguzi na teknolojia mpya ya habari. Aidha, programu hiyo iliangalia namna ya uandishi wa taarifa kuhusu serikali, uhuru wa vyombo vya habari na maadili ya uandishi wa habari. Msisitizo wa kipekee uliwekwa katika uandishi wa habari kuhusu afya na VVU/UKIMWI ili kujenga stadi za namna ya kuutaarifu umma kuhusu masuala muhimu yanayohusu afya nchini Tanzania.

Washiriki waliishi na familia mbalimbali zilizojitolea kuwapokea ili kujifunza hali halisi ya maisha ya familia za Kimarekani. Pia walitembelea jiji la Washington D.C. ambako walikutana na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi, wataalamu wa USAID kuhusu masuala ya vyombo vya habari na wawakilishi wengine mbalimbali wa serikali ya Marekani.

Hali kadhalika waandishi hao walipata fursa ya kuutembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani ili kujifunza zaidi kuhusu ushirikiano wa karibu baina ya nchi hizi mbili. Hili lilikuwa ni kundi la pili la waandishi wa habari kuhudhuria Programu ya Mabadilishano ya Waandishi wa Habari katika Chuo Kikuu cha Maine. Waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo hayo ni pamoja na Joyce Magoti (Media Solutions), Monica Luwondo (Tanzania Media Women’s Association), Simon Berege (Chuo Kikuu cha Tumaini), Deus Ngowi (New Habari Ltd) na Kamalamo S. Kamalamo (Changamoto). Wengine ni Simon Kivamo (Chama cha Waandishi wa Habari za UKIMWI Tanzania), Khalfan H. Said (The Guardian), Rachel Yusuf (Africa Media Group) na Levina Kato (Mwananchi).

Katika hafla iliyofanyika katika Ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam kila mshiriki alipatiwa kompyuta ndogo (laptop) zitakazowasaidia kutumia kikamilifu ujuzi walioupata katika kuwahudumia Watanzania.

Fedha zilizowawezesha waandishi hawa wa habari kushiriki katika programu hii ya mabadilishano zimetolewa na watu wa Marekani kama sehemu ya msaada wa Serikali ya Marekani kwa Tanzania wa zaidi ya shilingi za Kitanzania bilioni 750 katika mwaka huu wa fedha.

 
Article translated in: