Skip Navigation
You Are In: Home > Habari Kutoka Ubalozi > Kiswahili Press Releases > Kifo Cha Seneta Edward M. Kennedy
Skip Left Section Navigation

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

OFISI YA MSEMAJI WA IKULU
KIFO CHA SENETA EDWARD M. KENNEDY


Agosti 27, 2009

TAMKO LA RAIS WA MAREKANI

Senata Edward M. Kennedy hakuwa tu mmoja kati ya Maseneta mashuhuri na waliotoa mchango mkubwa sana katika zama zetu, bali pia mmoja kati ya Wamarekani waliojitoa mhanga kwa mafanikio makubwa kuilinda na kuiimarisha demokrasia yetu. Kwa zaidi ya kipindi cha nusu-karne, karibu kila sheria muhimu inayolenga kuimarisha haki za kiraia, afya na ustawi wa kiuchumi wa watu wa Marekani ilikuwa na jina lake na ilipitishwa kutokana na jitihada zake. Kwa kifo chake, sura muhimu katika historia ya Marekani imefikia mwisho.

Kama sehemu ya kumuenzi na kukumbuka mchango wa Seneta Edward M. Kennedy, kwa mamlaka niliyopewa na Katiba na Sheria za Marekani nina agiza kuwa bendera ya Marekani katika majengo na ofisi zote za Serikali ya Marekani ndani na nje ya nchi ipepee nusu mlingoti.

BARACK OBAMA

 
Article translated in: