Skip Navigation
Skip Left Section Navigation

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari

Wamarekani wavutiwa na ziara ya Mama Kikwete

Oktoba 03, 2006

Mke wa Rais wa Tanzania Mama Salma Kikwete alikutana na waigizaji wa kipindi maarufu kabisa duniani kinachowaelimisha watoto ambacho kinaitwa Sesame Street wakati alipotembelea New York hivi karibuni. Ziara hiyo iliwapa Mama Salma pamoja na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Margareth Sitta, fursa ya kujionea wenyewe kipindi hicho chenye ubunifu, ambacho huangaliwa na watoto katika nchi zaidi ya 120.

Mke wa Rais alizungumzia umuhimu wa kutoa elimu ya awali kabla ya watoto kufikia umri wa kuanza shule, na kusema kwamba matumizi ya lugha ya Kiswahili yatahakikisha ujumbe wa elimu unawafikia watoto na walezi wao kikamilifu. Kufanikiwa kwa utengenezaji wa vipindi vya Sesame Street vinavyoendana na mazingira ya nchi ya Afrika ya Kusini kumelihamasisha shirika la misaada la Marekani USAID kuanza kubuni mipango na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali ya kukileta kipindi hicho hapa Tanzania. Vipindi ambavyo hutengenezwa katika nchi mbalimbali huwa vinaandaliwa kukidhi mahitaji maalum ya maeneo hayo au nchi hizo. Kama ilivyokuwa wakati kikaragosi kutoka Afrika ya Kusini kinachoitwa Kami, ambacho kina virusi vya UKIMWI, kilipoingizwa kwenye tamthilia, kuna mipango ya kuhakikisha kwamba kipindi hicho kitatoa taarifa zinazohusiana na afya pamoja na maendeleo ya motto, taarifa ambazo zinaendana na mazingira halisi ya Tanzania. .

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa USAID Tanzania, Pamela White, “Shirika la USAID hivi karibuni lilifanya kazi pamoja na Misri ili kuongeza kikaragosi kingine kwenye maigizo hayo. Kikaragosi hicho chenye rangi ya waridi kina umri wa miaka minne na kinataka kuwa rubani wa ndege, daktari, na mhandisi – vyote kwa wakati mmoja! Kikaragosi hicho na marafiki zake wanabadilisha mtazamo kuhusu suala la elimu kwa wasichana, na wakati huo huo kinawasaidia watoto wote kujiandaa vizuri kufanikiwa shuleni. Mke wa Rais, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, pamoja na mimi tunataka kufanikisha kitu kama hicho hapa nchini Tanzania.” .

Akigusia mafanikio ya ziara ya wiki moja aliyoifanya Mke wa Rais nchini Marekani, Mkurugenzi wa USAID Tanzania Pamela White alisema, “Kwa kweli Wamarekani walivutiwa sana na Mama Salma. Kila mahali alipokwenda, alionekana mtanashati, akiongea vizuri, na alikuwa Balozi muhimu wa nchi ya Tanzania.” Aliongezea kwamba, “Wananchi wa Marekani, kuanzia wanafunzi wa miaka mitano wa shule ya msingi aliyoitembelea, hadi afisa mwandamizi wa taasisi mashuhuri ya Smithsonian Institution, walifurahishwa sana na ari pamoja na umakini wake.

- Translation -
This content is also available in English

- Mama Kikwete akutana na 'Cookie Monster' -
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Sitta, pamoja na Mkurugenzi wa shirika la misaada la Marekani, Pamela White, wakutana na Cookie Monster, karagosi la kipindi cha kuelimisha watoto cha Sesame Street. 
Enlarge - 461kb

Maelezo ya picha: Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Sitta, pamoja na Mkurugenzi wa shirika la misaada la Marekani, Pamela White, wakutana na Cookie Monster, karagosi la kipindi cha kuelimisha watoto cha Sesame Street.