Skip Navigation
Skip Left Section Navigation

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari

Mama Salma Kikwete ahamasisha kushiriki kwa Tanzania kwenye tamasha la kimataifa la utamaduni

Oktoba 17, 2006

Taasisi ya Smithsonian Institution nchini Marekani ina mkusanyiko mkubwa zaidi wa nyumba za makumbusho (museums) ulimwenguni, zilizo kwenye nchi moja – nyumba 17 za makumbusho pamoja na taasisi za utafiti. Tangu mwaka wa 1967, kituo cha utamaduni cha Smithsonian’s Center for Folklife and Cultural Heritage kimekuwa kinaandaa tamasha la utamaduni kila mwaka ambalo hutembelewa na zaidi ya watu milioni moja kutoka nchi za nje na Wamarekani milioni 30.

Maonesho ya taasisi hiyo huonesha sanaa na tamaduni kutoka maeneo mbalimbali ya taifa la Marekani na angalau nchi moja ya nje. Ngoma, muziki, hadithi, mapishi, kazi za mikono, na nyimbo ni sehemu ya tamasha la siku kadhaa ambalo hufanyika kwenye Washington Mall, ambalo ni eneo kubwa lenye bustani pamoja na majengo na minara ya kihistoria. Tamasha la Folklife Festival ni tamasha kubwa kuliko yote ya kitamaduni linalofanyika kila mwaka kwenye mji mkuu wa Marekani. Wakati wa ziara yake Septemba nchini Marekani, Mama Salma Kikwete alikutana na mameneja wa taasisi ya Smithsonian ili kuwashawishi kwamba Tanzania inastahili kupewa kipaumbele kushiriki kwenye maonesho hayo.

Mama Salma Kikwete, huku akionekana kama malkia kwenye mavazi yake ya Kiafrika, alisimama mbele ya maafisa hao na kusema: “Ninajua nchi nyingi huwatumia barua, taarifa na picha, lakini taifa la Tanzania limenituma mimi, Mke wa Rais, kuwashawishi kwamba Tanzania inastahili kuchaguliwa kushiriki kwenye tamasha la Folklife Festival. ” Timu ya taasisi ya Smithsonian ilifurahishwa sana na usemi huo.

Akifafanua kwamba Tanzania itakuwa ni mchango wa thamani kwenye tamasha hilo, Mama Salma Kikwete alionesha picha kadhaa kutoka Tanzania za michoro ya Tinga Tinga, vinyago vizuri vya Kimakonde, khanga na vikoi, vikapu, viungo na majengo ya Zanzibar, mapambo ya vito vya kitamaduni, pamoja na picha ya kuvutia ya video iliyoonyesha uzuri na upana wa mandhari mbalimbali za nchi ya Tanzania.

Huku wakiwa wamevutiwa na vitu hivyo vizuri vya kitamaduni, pamoja na ari ya Mama Salma Kikwete, mameneja wa tamasha hilo walimhakikishia Mke wa Rais kwamba Tanzania inakaribishwa kushiriki.

Akionesha kwamba hakatishwi tamaa na kipindi cha mpaka miaka miwili ya matayarisho, Mama Salma Kikwete alikishawishi kikosi cha taasisi ya Smithsonian kwamba, Watanzania watamudu kazi hiyo, na aliwaalika kuitembelea Tanzania 2007 ili kukutana na wananchi wa Tanzania na kujionea mwenyewe utamaduni wao, pamoja na historia yao.

- Translation -
This content is also available in English