Skip Navigation
Skip Left Section Navigation

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari

Mradi Mpya wa Elimu ya Mazingira Wazinduliwa

October 31, 2006

Mradi wa mazingira wa Roots and Shoots wa taasisi ya Jane Goodall Institute pamoja na Serikali ya Marekani leo Jumanne Oktoba 31, 2006 saa 4:30 asubuhi watazindua mradi mpya wa Elimu ya Mazingira kwa Shule za Msingi na Madrassa kwenye Shule ya Msingi ya Mtongani, Kunduchi. Mgeni wa heshima atakuwa Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Mazingira, Prof. Mark Mwandosya.

Mradi huu ni wa miaka miwili na unafadhiliwa na Serikali ya Marekani. Wanafunzi kutoka shule tano zitakazoshiriki, pamoja na wageni maalum zaidi ya 50 walioalikwa, wakiwemo Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Balozi wa Marekani, Mkurugenzi wa shirika la misaada la Marekani USAID, wawakilishi kutoka kwenye wilaya zinazohusika na mradi huu, na Rais wa taasisi ya Jane Goodall Institute, Marekani (JGI - USA), watakusanyika kushuhudia hotuba, maigizo, pamoja na upandaji wa mti.

Kwa mara ya kwanza, mradi ambao unalenga hususan vijana, utakuwa na jukumu la kubainisha nguvu itakayohusisha kwa pamoja elimu ya mazingira na mafunzo ya vitendo, ili kufanikisha mradi unaolenga na kuongozwa na vijana, ambao utashughulikia masuala yanayohusu elimu ya mazingira nchini Tanzania.

Mradi huu utahusisha zaidi ya wanafunzi 2,500 na waalimu 440 katika wilaya 11, zikiwemo wilaya nne kutoka Zanzibar. Kwa kushirikiana na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), mradi wa “Roots & Shoots wa taasisi ya JGI utawafikia pia wanafunzi 12,650 wa madrassa, pamoja na wanafunzi 12,650 wa shule za msingi. Aidha, waalimu 220 wa madrassa na waalimu 220 wa shule za msingi watapewa mafunzo ya Elimu ya Mazingira. Mafunzo hayo pia yatahusisha mbinu za kusambaza taarifa hizi ili ziwafikie pia waalimu na wanafunzi wengine, na jinsi ya kuanzisha na kusaidia miradi ya kutunza mazingira mashuleni, pamoja na vikundi vya Roots & Shoots.

Mradi wa Roots & Shoots wa taasisi ya Jane Goodall Institute ulianzishwa 1991, wakati kikundi cha wanafunzi 16 walipojiunga na kuanzisha Roots & Shoots, kwa lengo la kuwafundisha na kuwahamasisha vijana, na pia kusaidia kutayarisha viongozi wa baadaye wa taifa la Tanzania na dunia. Hadi sasa, mradi wa Roots & Shoots umefanikiwa kusajili zaidi ya wanachama 100,000 hapa nchini na kuenea katika nchi 96 ulimwenguni. Kwa kufanya kazi mashuleni na katika jamii, wanachama wake hutumia rasilimali kutoka duniani kote katika juhudi za kutunza na kuboresha mazingira yao asilia, pamoja na yale ya kijamii.

- Translation -
This content is also available in English