| - Translation - |
| This content is also available in English |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
USAID yasaidia semina ya sayansi kwa wasichana Zanzibar
Novemba 21, 2005
Semina ya wiki moja ya kuwahamasisha wasichana kuhusu masomo ya sayansi ilianza jana kwenye Chuo cha Walimu cha Nkrumah, Zanzibar. Hotuba ya ufunguzi ilitolewa na Bi. Mwanaidi S. Abdalla, Kaimu Katibu Mkuu katika Wizara ya Elimu Zanzibar. Semina hii inafadhiliwa na shirika la misaada la USAID kupitia mradi wake wa MKEZA (Mradi wa Kuboresha Elimu Zanzibar). Semina hiyo imeandaliwa na taasisi ya wanawake ambao ni wataalamu katika masuala ya elimu barani Afrika, Forum for African Women Educationalists (FAWE). Wasichana 60 na walimu 12 wanaowakilisha mikoa mitatu ya Unguja wamekaribishwa kushiriki.
Kwa kawaida, wasichana hawashiriki sana katika masomo ya hesabu na sayansi kama wavulana, na hivyo huwa hawafanyi vizuri katika masomo hayo kama wenzao wavulana. Hali hii pia inajitokeza nje ya shule katika sehemu za kazi ambako wanaume wengi zaidi hufanya kazi zinazohusiana na fani za sayansi kuliko wanawake. Semina hiyo itasaidia kuchochea mwamko kuhusu fani za hesabu na sayansi miongoni mwa wasichana, ili kurekebisha mapungufu haya.
Malengo ya semina hiyo ya sayansi ni:
Semina ya Unguja inafuatia semina iliyofana sana ambayo ilifanyika Pemba mwezi wa Septemba. Semina hiyo ambayo pia iliandaliwa na USAID, FAWE na MKEZA ilihusisha wasichana 40 na walimu 8 kutoka shule 8 za sekondari kisiwani humo. Tathmini ya semina ya Septemba ilionyesha kwamba asilimia 80 ya wasichana walitambua kwa mara ya kwanza umuhimu wa masomo ya sayansi na hesabu. Wanafunzi wasichana na wawakilishi wa shule za sekondari waliahidi kusaidia kuendeleza vikundi vya sayansi katika shule zao, huku mradi wa MKEZA na taasisi ya FAWE zikitoa misaada ya kiufundi na kufuatilia utekelezaji.
Semina hiyo ya sayansi inalenga hususan masomo ya baiolojia, kemia, fizikia na hesabu, na pia kuhusisha mada juu ya UKIMWI, utumiaji wa madawa ya kulevya, masuala ya jinsia na utunzaji wa mazingira, pamoja na jinsi ya kuendesha vikundi vya sayansi shuleni. Wasichana wote watapata fursa ya kutumia vifaa vya maabara, kufanya majaribio ya sayansi na kujadili masuala ya sayansi na mada kadhaa.



