| - Tafsiri - |
| This content is also available in English |
Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
Mradi Wa Rais Wa Marekani Wa Kudhibiti Malaria Tanzania Kuzinduliwa Leo Zanzibar
Desemba 19, 2005
Mradi wa Rais wa Marekani wa Kudhibiti Malaria Tanzania (PMI) unazinduliwa leo Disemba 19, katika uwanja wa Polisi wa Mahonda, Zanzibar. Mradi huu ulitangazwa na Rais George Bush mwezi Juni na kuidhinishwa na mkewe, Laura Bush pamoja na mke wa Rais wa Tanzania, Anna Mkapa jijini New York mwezi Septemba, ukiwa na lengo la kupunguza angalau asilimia 50 ya vifo vya watoto na wanawake wajawazito vinavyosababishwa na malaria katika Nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.
PMI ni mradi ambao unatekelezwa sehemu mbalimbali duniani kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo (USAID) na Taasis ya cha Kudhibiti Magonjwa (CDC). Ingawa ni ugonjwa unatibika na kuzuilika, Malaria ni ugonjwa unaoongoza kwa kusababisha vifo vya watoto wanaokadiriwa kufikia 80, 0000 kila mwaka nchini Tanzania.. Mradi huu unatoa fursa kwa Tanzania na nchi nyingine zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara kudhibiti malaria kikamilifu.
Jumla ya dola za Marekani bilioni 1.2 zimetolewa kwa nchi zipatazo 15 zilizo kusini mwa jangwa la Sahara kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. Tanzania ni mojawapo ya nchi tatu za awali zinazonufaika na mradi huu. Katika mwaka wa 2005/2006 Tanzania itafaidika kwa kupata jumla ya dola za Marekani milioni 11.5. Uzinduzi huu wa leo ni kielelezo cha juhudi za pamoja kati ya serikali ya Tanzania, serikali ya Mapinduzi Zanzibar, mashirika ya USAID na CDC, mfuko wa Global Fund, wahisani mbalimbali, taasisi zisizo kuwa za kiserikali, mashirika ya kijamii na kidini na sekta binafsi.
Malaria huenezwa kutokana na kuumwa na mbu ambao wana vimelea vya malaria. Kupitia PMI, Mradi wa Kudhibiti Malaria Zanzibar (ZMCP) utapata msaada kwa ajili ya visiwa vya Unguja na Pemba kwa ajili ya kuzuia na kudhibiti malaria katika nyanja zote.
Kwanza, Mradi huo utanzaa kwa kutoa na kusambaza vyandarua vya kudumu 240,000 kwa wanawake wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano ili kuzuia makundi yaliyo katika hatari ya kupata malaria yasiumwe na mbu. Vyandarua hivyo ni msaada uliotolewa kwa ushirikiano kati ya PMI na Mfuko wa Dunia wa UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria. Vyandarua hivyo, vitasambazwa kupitia kliniki za serikali. Taarifa za namna ya kupata vyandarua kudumu zitaolewa na Masheha au viongozi wa serikali za mtaa.
Mradi wa Kudhibiti Malaria Zanzibar chini ya ufadhili wa PMI utaratibu na kusimamia usambazaji na kampeni za uelimishaji kuhusu umuhimu wa vyandarua vya kudumu. (chandarua cha kudumu kina dawa inayotoka kidogo kidogo kwa kipindi kirefu hivyo kukipa chandarua kinga yenye uwezo wa kufukuza na kuua mbu. Chandarua kinadumu kwa miaka mitano na hakihitaji kuwekwa dawa). Dawa hiyo haina madhara kwa binadamu na imeidhinishwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Inakadiriwa kuwa zaidi ya matukio 420,000 ya malaria na vifo vipatavyo 2,500 vitazuiwa kwa kutumia vyandarua hivi.
Pili, PMI itashirikiana na Mradi wa kuzuia malaria wa Zanzibar (ZMCP) kunyunyiza dawa majumbani ambayo kitaalam inajulikana kama IRS (Indoor Residual Spraying). Utekelezaji wake utaanza mwaka ujao ambapo nyumba zitanyunyiziwa dawa ya kuua mbu waenezao malaria ambayo haina athari kwa binadamu na mazingira kabla ya kuanza kwa majira ya mvua za masika.
Tatu, jambo la tatu ni kwamba Watanzania wana sio wepesi kutafuta tiba ya homa kali hasa kwa watoto wadogo, yaani wanachelewa kuwapeleka watoto wenye homa na maradhi mengine ambayo ni dalili za malaria kwa wauguzi na wataalamu. Kufuatia hali hii, PMI kupitia ZMCP, itaelimisha na kushawishi wananchi wajenge utamaduni wa kuwahi kutauta na kupata tiba katika kipindi kisichozidi saa 24 tangu dalili za malaria zinapoibuka. Msisitizo na mkazo mkubwa utaelekezwa na kwa wanawake wajawazito na watoto walio chini ya miaka mitano. Tiba kamilifu ya malaria itatolewa kwa kutumia dawa mchanganyiko katika zahanati za serikali ili kudhibiti kuenea kwa vimelea vya malaria. Hata hivyo, serikali itasaidiwa katika jukumu hili na PMI kutokana na gharama zake kwa kuweka vifaa vya maabara vya kuchunguza vimelea vya malaria katika zahanati zake vijulikanavyo kitaalam, kama (Rapid Diagnostic Tests). Vifaa hivi havihitaji mafunzo ya muda mrefu kumudu matumizi yake na vinatoa majibu yaliyo sahihi zaidi na katika muda mfupi usiopungua dakika 15. vifaa hivi vinahitajika sana Zanzibar kutokana na ukweli kwamba matukio mengi ya homa katika visiwa hivi hayachunguzwi na wakati mwingine husababisha vifo visivyo na sababu.
Nne, wanawake wajawazito wanashauriwa kutumia dawa za kuzuia malaria (intermittent preventative treatment -IPT), katika utaratibu huu, wanapatiwa dozi ya dawa ya malaria ambayo ina uwezo wa kuwakinga wao wenyewe na watoto dhidi ya malaria.
Waswahili wana usemi wao usemao “usilenge ndege wawili kwa jiwe moja” lakini sie leo twataka kulenga ndege wawili kwa jiwe moja kwa kuzindua mradi wa PMI na kampeni ya Kataa Malaria (Reject Malaria). Hivyo basi, Mradi wa Kudhibiti Malaria Zanzibar kwa kushirikiana na PMI unawaalikeni nyote katika ‘Bonanza la Kataa Malaria’ shamrashamra hizi za siku moja zitaanza na mkutano wa waandishi wa habari saa 5.30 na kuendelea na matukio mengine ambayo ni pamoja na maonyesho, maigizo ya kuelimisha jamii namna ya kuzuia malaria, muziki, ngoma, michezo na chakula pamoja na hotuba kutoka kwa viongozi mbalimbali akiwamo Rais wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa Aman Abeid Karume, na Mkurugenzi wa USAID Tanzania, Pamela White.. Mpango wa PMI una mkakati wa kuanza kusaidia Mradi wa Kudhibiti Malaria Tanzania kuanzia mwaka 2006.



