Skip Navigation
Skip Left Section Navigation

Speeches

Mkutano na waandishi wa habari kuhusu Ripoti ya Mwaka ya Mpango wa Dharura wa Rais Bush Kupunguza Makali ya UKIMWI [PEPFAR]

March 3, 2006

  • Asante John, na karibuni nyote. Asanteni kwa kupata nafasi ya kuja hapa. Tunathamini sana kazi inayofanywa na vyombo vya habari, na mimi mwenyewe nina shauku ya kuwasaidia katika shughuli zenu za uandishi kuhusu janga la UKIMWI…


  • Lakini kuna nini tena cha kusema kuhusu UKIMWI ambacho bado hakijasemwa? Je, unawezaje kuzifanya taarifa ziendelee kuvutia na kuripotiwa kwenye vyombo vya habari?


  • Taarifa hizi zimekuwa nasi kwa muda mrefu – hapa Tanzania ugonjwa huu uliripotiwa kwa mara ya kwanza 1983, kwa hiyo ninyi – wanahabari – mmekuwa mkiandika taarifa hizi kwa muda wa zaidi ya miongo miwili.


  • -

  • Je, unawezaje kuwaelewesha watu? Maneno gani yanaweza kuelezea janga hili ambalo limeathiri maisha ya watu zaidi ya milioni 40 ambao wanaishi na virusi vya UKIMWI?


  • Je, ni rahisi kuelewa ukweli kwamba zaidi ya watu milioni moja na nusu kati ya hao ni Watanzania – au kwamba idadi hii inaongezeka kila siku?


  • Na vikwazo haviishii hapo tu, janga la UKIMWI linashindania nafasi kwenye vyombo vya habari na taarifa nyingine nyingi za kuvunja moyo ambazo utatuzi wake ni mgumu. Ukame, uwezekano wa kutokea janga la njaa, uvamizi wa viwavijeshi, na mengineyo.


  • -

  • Kwa hiyo UKIMWI ni taarifa za zamani, ni mgumu kueleweka, na unashindania nafasi na taarifa zingine nyingi.


  • …na hata hivyo kila mmoja wenu anafanya bidii kuhakikisha kwamba ugonjwa huo hausahauliki, huku tukiendelea kukabiliana na changamoto zinazohusu taarifa zingine.


  • -

  • Kuwa kwenu hapa ni ushahidi tosha kuhusu juhudi zenu. Wakati huu wa kutoa ripoti yetu ya mwaka kwa Baraza la Congress juu ya ‘Juhudi zetu za kudhibiti kuenea kwa UKIMWI duniani,’ ningependa kuwapongeza kwa juhudi zenu za dhati katika kazi hii muhimu.


  • Kila mmoja wenu ametoa mchango wake, na kila moja wenu anastahili pongezi.


  • …hebu geuka na uangalie. Wewe na wenzako mlio hapa leo hamkuandika tu taarifa kuhusu janga la UKIMWI, mmechukua hatua muhimu zaidi ya kutaarifu na kuelimisha kupitia kazi yenu.


  • Na taarifa mnazosambaza zinasaidia kweli – zinaokoa maisha ya binadamu.


  • -----

  • Leo tutasikia kutoka kwa kikundi cha watu ambao wana bidii kama ninyi, lakini wamechagua kuonyesha juhudi zao kwa njia tofauti kidogo.


  • Watu hawa wanatoka hapa Tanzania, Marekani, kwa kweli wanatoka duniani kote. Hawa ni wataalamu wa masuala ya afya, watendaji – watu wenye bidii kutoka fani mbalimbali.


  • -

  • Wamekusanyika hapa leo kwa matumaini ya kuwasaidia ninyi. Wanatarajia kufanya hivyo kwa kuelezea juhudi zao hapa nchini za kujaribu kudhibiti kuenea kwa UKIMWI.


  • Na wataelezea juhudi zao za kuwasaidia watu wengi – kwa mfano watoto yatima pamoja na wale wanaoishi katika mazingira magumu – ambao maisha yao yameathiriwa na kuenea kwa UKIMWI.


  • -

  • Wangependa kuwaelezea shughuli wanazozifanya kwa sababu wanajua kwamba kuwasaidia ninyi ni muhimu katika kufanikisha kazi zao.


  • Wameamua kuwa hapa leo kwa sababu kama yenu – kwa sababu wanaelewa kwamba kuwasaidia ninyi kueneza ujumbe ni muhimu sana kwa vita yetu wote dhidi ya janga la UKIMWI.


  • ---------

  • Katika kipindi cha miaka michache iliyopita, kitu cha ajabu sana kimetokea – tumeona jinsi mataifa yanavyounganisha nguvu zao katika juhudi za kudhibiti kuenea kwa UKIMWI.


  • Marekani peke yake imebeba jukumu hili kwa kufadhili mpango mkubwa wa afya kuliko yote ambayo imewahi kutekelezwa na nchi moja katika historia.


  • Ingawa tumefanya jambo muhimu sana, kwa vyovyote vile hatuko peke yetu. Taasisi ya Global Fund
    – mshiriki mwingine mkubwa wa TACAIDS hapa nchini
    – ni kubwa zaidi.


  • Mfuko huo unafadhiliwa na nchi nyingi – ikiwemo tena Marekani – pamoja na wahisani wengine duniani kote.


  • -

  • Katika kipindi cha miaka michache iliyopita, kikwazo kikubwa – kikwazo cha upungufu wa fedha – kimeondolewa kwa kiasi kikubwa.


  • Leo hii, wengi walioathirika na UKIMWI wanaona faraja kujua kwamba kuna uhakika wa fedha kupatikana, na kwamba dawa za kupunguza makali ya UKIMWI zinapatikana au zitapatikana hivi karibuni.


  • -

  • Hizi sio tu taarifa njema kwa waathirika wa UKIMWI, lakini ni muhimu pia kwa wale kati yetu ambao wameamua kuwa hawataki kujua kama wameathirika au la:


  • Tunaweza sasa kwenda kupimwa – tukiwa na uhakika kwamba kwa mara ya kwanza kabisa nchini Tanzania – ni bora kujua kama sisi ni wagonjwa.


  • Hii ni kwa sababu, kwa mara ya kwanza kabisa nchini Tanzania, kila mtu ana uhakika wa kupewa tiba kama ataonekana ana virusi vya UKIMWI.


  • -

  • Na sasa hivi, kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miongo miwili, akina mama walioathirika wanaweza kuzuia virusi kuwaambukiza watoto wao


  • …lakini hii itawezekana tu kama wanajua. Kujua ni muhimu sana katika enzi hizi.


  • ---------

  • Kwa hiyo tunarudi tena kwenu, wawakilishi wa vyombo vya habari, na umuhimu wa ninyi kuwa hapa leo kueneza ujumbe.


  • Ujumbe huu unahusu hatua za msingi za kujikinga, na wajibu wa jamii tulio nao kila mmoja wetu kwenda kupimwa.


  • Ujumbe huu unahusu umuhimu wa kutafuta tiba – na hatua sahihi za kuchukuliwa wakati wa kutoa huduma ya matunzo.


  • Ujumbe huu unahusu kutoa elimu ya kuondoa unyanyapaa na kuwakubali wale ambao mzigo wao ni kuishi na ugonjwa wa UKIMWI.


  • Na mafanikio ya kuuwezesha ujumbe huo usikike yako hasa mikononi mwa vyombo vya habari. Huu ndio wajibu wenu muhimu.


  • ---------

  • Ni matumaini yetu sisi, wawakilishi wa mpango wa Rais wa kupambana na UKIMWI, mpango wa PEPFAR, kuendelea kuwapa ninyi taarifa juu ya shughuli tunazozifanya – na tunazotarajia kuzifanya mwaka huu
  • – ili na ninyi mkauelimishe umma, ili uwe na taarifa kamili.


  • Ni matumaini yangu kwamba mtaondoka hapa asubuhi ya leo mkijua kuwa mmetumia muda wenu vizuri pamoja nasi; mkiwa na uelewa mzuri zaidi; mkiwa mmejitayarisha vizuri zaidi kuelimisha, kwa mtazamo mpya juu ya kazi yetu.


  • Lakini la muhimu zaidi, tunatumaini kuwaacha na hamasa mpya ya kueneza ujumbe. Asanteni, na nawashukuru tena kwa kuwa nasi siku ya leo.