speeches
Hotuba fupi ya Kaimu Balozi Purnell Delly kwenye uzinduzi wa kondomu ya 'Dume', Mirerani
Venue: Mirerani, Simanjiro District, Manyara Region. April 8, 2006.
- Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bwana Mr. Edward Lowassa
- Mkurugenzi wa shirika la USAID nchini Tanzania, Bi. Pam White
- Viongozi wa Serikali ya Tanzania
- Waheshimiwa Wabunge
- Wawakilishi wa migodi
- Wawakilishi wa vyombo vya habari
- Mabibi na Mabwana
- I am happy to be here today [Tafsiri: Nina furaha kuwa hapa leo]
- Leo tunazindua mradi wa mamilioni ya dola kuhakikisha kwamba kondomu zinapatikana kwa wingi
- na zinawekwa ili ziweze kuonekana katika sehemu na wakati zinapohitajika kutumiwa.
- Mwaka jana, mpango wa dharura wa Rais wa Marekani kupunguza makali ya UKIMWI ulifadhili huduma zinazohusiana na utoaji wa kondomu, na huduma hizi ziliwafikia watanzania zaidi ya milioni 4.
- Mwaka jana pia tulitoa kondomu zaidi ya milioni 18 na nusu.
- Kwa ujumla, mwaka huu Serikali ya Marekani itatumia zaidi ya shilingi bilioni 130 kusaidia shughuli za kuzuia maambukizi ya UKIMWI, matunzo na tiba kwa wagonjwa nchini Tanzania -
- lakini leo hatukuja hapa kuzungumzia juu ya Serikali ya Marekani…
- Tuko hapa kuzungumzia juu ya kondomu….
- Mnaelewa ninachokizungumzia, au siyo? Soksi?
- Je, mnafahamu watu husemaje kuhusu soksi? ‘Huwezi kuvaa koti la mvua wakati wa kuoga! Au siyo?’
- Hebu ngoja niwaelezeni hadithi moja kuhusu rafiki yangu aliyekuwa amejiwekea akiba ya pesa ili aweze kununua gari.
- Hakuwa na fedha za kutosha kununua gari nzuri. Fedha alizokuwa nazo zilitosha tu kununulia gari ya bei ya chini. Kwa hiyo alikuwa na wasiwasi kwamba angetumia pesa zake zote na mwishowe agundue kuwa gari hilo lilikuwa na tatizo kubwa.
- Alihisi angeweza kupoteza kila kitu kama muuzaji akimdanganya kuhusu gari lake. Kwa hiyo akawaza, akisema ‘ninahitaji kumtafuta mtu fulani ambaye nitamkabidhi pesa zangu na kumwambia: ‘Usimpe pesa zangu muuza gari mpaka nimehakikisha kwamba gari halina matatizo yoyote.’
- Kumbe muuza gari naye alikuwa na mawazo yale yale kama rafiki yangu. Mama yule akajiuliza, ‘Hivi huyu mtu ninamfahamu vizuri kweli? Kwa nini nimuamini? Ananiambia eti pesa zake ni safi, lakini labda ni chafu kuliko gari langu kuukuu; pengine ni za bandia.
- Kwa hiyo wakakubaliana kumtumia mtu ambaye wote wawili walikuwa wanamfahamu na kumwamini. Yule mama akampa mtu huyo funguo za gari lake na rafiki yangu akamkabidhi pesa zake.
- Ninaamini mmekuwa mkiifuatilia hadithi hii kwa makini, na ninafikiri mmetambua jina la mtu huyu ambaye wote wawili walikuwa na imani naye na hivyo kumweka katikati yao.
- Mnajua mtu huyo ni nani? Mnafahamu ni nani aliyehakikisha kwamba makubaliano kati yao hayana madhara kwa upande wowote…?
- DUME! …sawa kabisa, ni DUME.
- Asanteni sana, na msisahau, mara zote mnapoweka DUME kati yenu hakuna anayedhurika!