Skip Navigation
Skip Left Section Navigation

Kiswahili Speeches

Hotuba ya Balozi wa Marekani nchini Tanzania Bw. Michael Retzer Katika kuadhimisha siku ya UKIMWI duniani

Desemba 1, 2005


•Kiwango cha juu cha kujiepusha na ngono:Vijana zaidi wameripotiwa kujizuia kufanya ngono angalau kwa mwaka mmoja; na

•Kuongezeka kwa matumizi ya kondomu: Wanawake wanaojihusisha na shughuli hatari za ngono wamekuwa wakitumia kondomu zaidi kwa sasa.

• Habari njema ni kwamba mbinu hiyo hiyo iliyobadilisha upepo wa UKIMIWI nchini Kenya inaweza kufanya kazi hapa pia.

• Ukweli kwamba sisi sote tulio katika mkusanyiko huu leo kunaashiria dhamira yetu ya pamoja ya kushinda vita hii. Tunahitaji kuendelea na dhamira hii tukiwa na mikakati mahsusi ili kutia moyo dhana ya ABC hapa nchini Tanzania

• Mwisho, naomba nimalizie kwa kutoa shukurani zangu kwa TACAIDS na wale wote waliohusika katika kuandaa tukio hili kwa juhudi zao kubwa za kutuleta leo hapa sisi sote pamoja. Pia ningependa kuchukua fursa hii kuipongeza serikali ya Tanzania kwa uongozi, juhudi na hatua inazochukua katika kupambana na tatizo zima la UKIMWI. Nina matumaini ya kuendelea kufanya kazi kwa karibu na pamoja na serikali, wafadhili, mashirika na watu wa Tanzania ili hatimaye kutokomeza kabisa gonjwa hili la UKIMWI.

• Kwa pamoja tunaweza kutimiza ahadi na kuzuia UKIMWI. Asanteni sana.