Skip Navigation
Skip Left Section Navigation

Speeches

Salaam za Eid-el-Haj kutoka kwa Rais Bush

Desemba 19, 2007

Ninawatumia Waislamu wote salaam za kheri wakati huu wa siku kuu ya Eid-el-Haj.

Wakati wa Eid el-Haj, Waislamu ulimwenguni kote wanatafakari kuhusu imani thabiti ya Ibrahim kwa Mungu wakati alipotakiwa kumtoa mtoto wake sadaka. Siku nne hizi ni wakati wa Waislamu kuenzi utii wa Ibrahim kwa kusherehekea pamoja na familia na marafiki na kutoa shukrani kwa Baraka nyingi za Mwenyezi Mungu. Siku kuu hii pia husaidia kuhakikisha kuwa vizazi vijavyo vinashirikishwa maadili muhimu ya moyo wa huruma na wa kujitoa.

Marekani ni taifa la imani nyingi, na jamii yetu inastawishwa na wananchi wenzetu Waislamu. Moyo wa huruma, ukarimu na urafiki unaodhihirishwa na Wamarekani Waislamu wakati wa sherehe hii muhimu na wakati wote vimechangia kulipa Taifa letu nguvu na uhai. Hebu wote wanaosherehekea Eid-al Haj wafurahie upendo na faraja wakati wa siku kuu hii iliyojaa furaha.

Mke wangu Laura na mimi tunatuma salaam za kumbukumbu wakati wa sherehe hii muhimu.

GEORGE W. BUSH